Mkuu wa Wilaya ya Mpanda, Paza Mwamlima, ameagiza kuwa mtu yeyote atakayeugua ugonjwa wa kipindupindu akitibiwa na kupona, atafikishwa mahakamani kujibu kosa la kukiuka taratibu za afya na kuugua ugonjwa huo.
Mwamlima alitoa agizo hilo juzi wakati wa uzinduzi wa usafi wa mazingira na upandaji miti uliofanyika eneo la Kituo Kikuu cha Mabasi yaendayo mikoani Manispaa ya Mpanda mkoani Katavi.
Alisema yeyote atakayeugua ugonjwa wa kipindupindu wilayani Mpanda, atapatiwa matibabu, lakini akishapona, atashtakiwa kwa kukiuka kanuni za usafi.
Mwamlima alisema ugonjwa wa kipindupindu husababishwa na uchafu, hivyo kama mazingira ni masafi, mtu hataugua maradhi hayo.
Aliongeza kuwa wajibu wa kila mtu kuishi kwenye mazingira safi na kuuchukia uchafu ili kuepuka magonjwa ya mlipuko.
Mkuu huyo wa Wilaya amepiga marufuku baa kufunguliwa muda wa kazi na kucheza bao na watu kushinda kwenye vijiwe vinavyouza kahawa.
Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Dk. Ibrahim Msengi, amewaagiza wananchi wa manispaa hiyo kuhakikisha maeneo yao ya kuishi na wanayofanyia shughuli za biashara yanakuwa katika hali ya usafi.
Alisema kila Jumamosi wananchi wa manispaa hiyo wahakikishe siku hiyo wanaitumia kufanya usafi kwenye mitaa yao na kwa Jumamosi ya kwanza ya mwezi, itakuwa inatumika kwa ajili ya manispaa nzima ya Mpanda.
KUJIUNGA NA KINYANG'ANYIRO CHA PIKIPIKI AINA YA BOXER BONYEZA PICHA CHINI YA MANENO HAYA NA UIBUKE MSHINDI,BONYEZA MARA NYINGI UWEZAVYO KUIBUKA MSHINDI;
Post a Comment