Uteuzi wa Wabunge wa Viti Maalum Wapelekea Viongozi Wa Chadema Kujiuzulu

KUJISHINDIA MAMILIONI KATIKA DROO HII BONYEZA HAPA CHINI UJIUNGE KATIKA BAHATI NASIBU,NA ILI UIBUKE MSHINDI HAKIKISHA KILA SIKU WABONYEZA PICHA CHINI YA MANENO HAYA;

Viongozi wa ngazi za juu mkoani Rukwa akiwemo aliyekuwa mwenyekiti wa Chama hicho ngazi ya Mkoa, Zeno Nkoswe wametangaza kujiuzulu nafasi zao kufuatia kutoridhishwa na uteuzi wa wabunge wa viti maalum uliofanywa na viongozi wa chama hicho ngazi ya Taifa.
 
Viongozi hao wa Baraza la Chadema wameeleza kuwa mbunge wa viti maalum aliyeteuliwa alikuwa wakala wa TLP na sio Chadema kama walivyodai.

“Aliyeteuliwa mpaka sasa ni yule aliyekuwa wakala wa TLP. Kwahiyo huyo anaweza asiwe mbunge wa viti maalum wa Chadema akawa mbunge wa viti maalum wa TLP,” alisema Nkoswe na kuongeza kuwa Baraza hilo lilimpendekeza kada wa Chadema Sumbawanga Mjini lakini haikuwa hivyo.
 
Katika hatua nyingine, viongozi hao wamesema kuwa uongozi wa ngazi ya Taifa walishindwa kutimiza ahadi zao za kuwalipa mawakala waliosimamia uchaguzi katika maeneo hayo.
 
Walisema kuwa licha ya kuorodhesha majina ya mawakala hao ambao wamekuwa wakisubiri fedha kutoka makao makuu, fedha hizo hazikuwasilishwa kwao hivyo kuwafanya viongozi hao kugombana na mawakala hao.
KUJIUNGA NA KINYANG'ANYIRO CHA PIKIPIKI AINA YA BOXER BONYEZA PICHA CHINI YA MANENO HAYA NA UIBUKE MSHINDI,BONYEZA MARA NYINGI UWEZAVYO KUIBUKA MSHINDI;

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright UDAKU WA DUNIA Published.. Blogger Templates
Back To Top