SIRI YAFICHUKA...TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI YA MVAA RAIS JK KWA KAULI YAKE YA JANA ILIYOZUA SINTOFAHAMU KWA WANANCHI

KUJISHINDIA MAMILIONI KATIKA DROO HII BONYEZA HAPA CHINI UJIUNGE KATIKA BAHATI NASIBU,NA ILI UIBUKE MSHINDI HAKIKISHA KILA SIKU WABONYEZA PICHA CHINI YA MANENO HAYA;

Rais Jakaya Kikwete, akikabidhiwa Mwenge wa

Dar es Salaam. Kauli ya Rais Jakaya Kikwete aliyoitoa jana na kukosea idadi ya wapigakura walioandikishwa kushiriki uchaguzi mkuu wa mwaka huu, imeongeza idadi ya wananchi waliopiga simu kwenye kituo maalumu cha huduma kwa wateja cha Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).
Akiwa kwenye kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Mwalimu Julius Nyerere, aliyekuwa rais wa kwanza wa Tanzania, yaliyofanyika kitaifa mjini Dodoma Rais Kikwete alisema idadi ya wapigakura wanaostahili kwa Tanzania Bara ni milioni 28 na visiwani ni zaidi ya laki tano.
Kauli hiyo inakinzana na idadi iliyotangazwa na NEC mapema wiki hii ambayo ni milioni 22.75 hivyo kuzua sintofahamu miongoni mwa wananchi juu ya idadi halisi ya Watanzania watakaoshiriki uchaguzi hapo Oktoba 25. Ingawa baadaye Ikulu ilirekebisha kauli hiyo kupitia vyombo vya habari, wadau walitaka ufafanuzi kutoka NEC.
Mkuu wa Kitengo cha Habari NECo, Clarence Nanyaro amelieleza gazeti la Mwananchi kuwa kituo hicho kimezidiwa na idadi ya simu zinazoingia kiasi cha kupoteza ufanisi wake wa kutoa huduma inayostahili hivyo kuhitaji matengenezo madogo.
“Mwitikio umekuwa mkubwa sana kuliko ilivyotazamiwa. Tangu uzinduzi ulipofanyika leo saa 5:00 asubuhi simu 2,400 zilipokelewa. Na jana, mpaka saa 7:00 zilizopokelewa ni 3,010. Mashine imepoteza uwezo wake na tunafanya jitihada za kuirekebisha ili iendelee na kazi.
Miongoni mwa simu nyingi zinazopokelewa ni zile zinazotaka ufafanuzi juu ya kauli ya Rais Kikwete aliyoitoa jana. Tunaendelea kuwaelimisha wananchi kwamba idadi kamili ni ile iliyotangazwa na tume na si vinginevyo.”
Hata hivyo tume imewataka wananchi kuendelea kupiga namba 0800 782 100 ili kupata ufafanuzi wa masuala mbalimbali yanayohusiana na uchaguzi mkuu lakini wanaweza kutoa taarifa juu ya jambo linalokiuka maadili au kuvunja sheria za nchi kuelekea siku ya uchaguzi.
KUJIUNGA NA KINYANG'ANYIRO CHA PIKIPIKI AINA YA BOXER BONYEZA PICHA CHINI YA MANENO HAYA NA UIBUKE MSHINDI,BONYEZA MARA NYINGI UWEZAVYO KUIBUKA MSHINDI;

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright UDAKU WA DUNIA Published.. Blogger Templates
Back To Top