Utata Watawala Kifo cha Ghafla Cha Msemaji Wa Madereva, Rashid Saleh

KUJISHINDIA MAMILIONI KATIKA DROO HII BONYEZA HAPA CHINI UJIUNGE KATIKA BAHATI NASIBU,NA ILI UIBUKE MSHINDI HAKIKISHA KILA SIKU WABONYEZA PICHA CHINI YA MANENO HAYA;

Aliyekuwa Katibu na Msemaji wa Chama cha Madereva, Rashid Saleh amefariki dunia ghafla huku chanzo cha kifo chake kikizua utata miongoni mwa wananchama wa chama hicho na wananchi.

 

Taarifa za awali kifo cha Rashid Swaleh zilielza kuwa alifariki baada ya kuugua ghafla ugonjwa ambao bado  haujabainika.

 

Madereva na wananchi wengine walifika katika hospitali ya Muhimbili wakiwa na majonzi makubwa huku wakisubiri mwili huo wa marehemu upimwe ili kubaini chanzo cha kifo chake.

 

Baadhi ya madereva waliozungumza na waandishi wa habari walieleza kusikitishwa na msiba huo wa ghafla na kueleza kuwa huenda msemaji wao aliyekuwa anapigania kwa nguvu zote haki zao amenyamazishwa.

 

“Sisi kama madereva hatutakubali, kama kosa lake yeye ni kutetea haki za watu, hili ni tatizo,” alisema mmoja wa madereva hao aliyejitambulisha kwa jina la Shaban Mdem.

 

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadick alifika katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili na kuwataka madereva hao kutokata tama bali waendelee kudai haki zao huku wakisubiri majibu ya madaktari kubaini chanzo cha kifo cha msemaji wao.

 

“Hii isiwakatishe tamaa kuendelea kudai haki zenu ambazo ni za msingi kutoka kwa ajili wenu,” alisema huku akiwasihi kutofifishwa moyo katika kutafuta haki zao za msingi.

KUJIUNGA NA KINYANG'ANYIRO CHA PIKIPIKI AINA YA BOXER BONYEZA PICHA CHINI YA MANENO HAYA NA UIBUKE MSHINDI,BONYEZA MARA NYINGI UWEZAVYO KUIBUKA MSHINDI;

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright UDAKU WA DUNIA Published.. Blogger Templates
Back To Top